HUKU ‘NDOA’ YAKE NA UWOYA IKITIKISA…DOGO JANJA, MIJIMAMA SIRI 4 ZAVUJA!
Msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’.
SIKU zinakwenda kwa kasi kwani ni ‘majuzi’ tu zilisambaa taarifa za dogo anayefanya poa kwenye Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ kuwa alifunga ndoa isiyokuwa na vithibitisho na staa mkubwa wa Bongo Movies, Irene Pancras Uwoya. Nyuma ya tukio hilo lililotikisa vilivyo, kuna siri nzito ambazo zimefichuka juu ya Dogo Janja kupendwa na mastaa waliomzidi umri ‘majimama’, Ijumaa lilidokezwa.
Staa mkubwa wa Bongo Movies, Irene Pancras Uwoya akifanya mambo yake na anayesemekana kuwa mume wake Dogo Janja.
TUFUATANE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho ni mchambuzi wa habari za mastaa Bongo, tukio la wawili hao lina utata mkubwa kwani linavyoonekana ni la kutafuta ‘kiki’, ama ya sinema mpya ya Uwoya au wimbo mpya wa Dogo Janja.
…Akiwa na Shilole.
SIRI YA KWANZA
“Ninavyojua hakuna ndoa pale, namjua vizuri Uwoya, kwanza amezaliwa mwaka 1988 hivyo anakaribia umri wa miaka 30 na Dogo Janja amezaliwa mwaka 1997 na ana umri wa miaka 20. “Unajua Kibongobongo, wanaume wengi wamewazidi umri wake zao.
Ishu ya wanawake kuwazidi umri wanaume imeibuka kwenye kizazi tulichonacho na ndiyo maana uhusiano haudumu kwa sababu utakuta ‘mjimama’ mtu mzima anakuwa na ‘mtoto’ au ‘kiserengeti boi’ ambaye bado ana mambo mengi ya ujana. “Hata hivyo, kuna watu wanaamini kuwa umri ni namba tu na mapenzi ya kweli hayajali umri.
Dogo Janja na Agnes Masogange.
Ninachojua Dogo Janja na Uwoya ni washkaji tu,” kilisema chanzo hicho na kuongeza: “Kinachofanyika kuna watu wameamua kucheza na akili za Wabongo wasiokuwa na uwezo wa kuhoji, lakini pale hakuna ndoa. Na kama kweli kuna ndoa ninyi (Global) waambieni Uwoya na Dogo Janja waoneshe cheti cha ndoa.
“Kibaya zaidi hii ishu imeshirikisha watu wengi wenye heshima zao kama akina Madee, lengo likiwa nikutengeneza kiki kwa sababu kiki za Dogo Janja zilianza muda mrefu tangu jamaa huyo alipodai kuwa anamzimikia Uwoya tangu akiwa mdogo alikuwa anammezea mate runingani. “Huo ndiyo ukweli kwa sababu wakati Uwoya akiwa tayari ni staa miaka kumi iliyopita, Dogo Janja bado alikuwa shule ya msingi.”
CREDIT :Global publishers
Post a Comment