Header Ads

Yaya Toure Adai Furaha Yake ni Kushinda Taji la Ligi Kuu ya Mabingwa Barani Ulaya


Nyota wa Manchester City Yaya Toure amesema anatamani kutwaa ubingwa wa UEFA akiwa na timu hiyo ili kukamilisha ndoto yake.

Toure amedai furaha pekee anayoitamani ndani ya kikosi cha Manchester City ni kushinda taji la Ligi ya mabingwa barani Ulaya kwani  ndio kombe pekee ambalo hajafanikiwa kutwaa akiwa Etihad.
Yaya Toure hadi sasa ametwaa makombe mawili ya EPL, mawili ya EFL pamoja na moja la FA hivyo anaona kama hadaiwi chochote kutoka nchini England zaidi ya ubingwa wa Ulaya.

Raia huyo wa Ivory Coast ameshawahi kutwaa ubingwa wa UEFA akiwa na FC Barcelona mwaka 2009, hivyo anahitaji taji lake la pili la Ulaya. 

No comments