Header Ads

Watu Milioni 3 Wamo Hatarini ya Kufaa Nja DRC

Watu Milioni 3 Wamo Hatarini ya Kufaa Nja DRC


Umoja wa mataifa unasema kuwa zaidi ya watu milioni tatu wamo katika hatari ya kufa njaa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kiongozi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia mpango wa chakula Duniani- WFP, ametoa wito wa msaada wa dharura wa kimataifa, ili kumaliza matatizo ya baa la njaa, nchini DR Congo.

David Beasley, ambaye anafanya ziara yake ya kwanza kabisa, katika jimbo linalokumbwa na msukosuko wa mapigano na uasi la Kasai, ameiambia BBC kuwa, zaidi ya watu milioni tatu, wanakabiliwa na baa la njaa.

Anasema kwamba, timu ya wafanyikazi wake, wameshuhudia watoto ambao wanakabiliwa na matatizo ya utapia mlo, huku mamia kwa maelfu yao, wakiwa katika hatari ya kufa, katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo, ikiwa msaada hautawafikia.

Mapigano mabaya yalianza katika jimbo hilo la Kasai mwezi Agosti mwaka 2016, baada ya kiongozi mmoja wa kitamaduni kuuwawa, katika mapigano na wanajeshi wa kulinda amani.
Ghasia mpya imesababisha mauwaji ya watu elfu tatu na kuwafurusha zaidi ya watu milioni moja, wengi wao wakiwa ni watoto kutoka nyumbani kwao. 

No comments