Header Ads

Wakati dunia ikikumbuka kustaafu kwake, haya ni mambo 15 ya kufahamu kuhusu Pele


Ni uzao wa mshambuliaji wa kikosi cha Brazil cha miaka ya 1930’s – João Ramos do Nascimento na mwanamama Celeste Arantes. 
1.Ni baba wa watoto sita, Sandra Machado, Kelly Cristina, Flávia Kurtz, Edinho, Joshua na Celeste. 
2.Inasadikika ndio mchezaji bora wa wakati wote wa soka, akiwa na rekodi ya kucheza jumla ya mechi 1281 na kufunga magoli 1363. 
3.Ameshinda ubingwa wa dunia na Brazil mara 3 na Copa America mara 1. •Mfungaji bora wa muda wote wa Brazil (Magoli 95)
4.Ana rekodi ya dunia ya kufunga hat tricks 92
•Mfungaji mdogo zaidi katika michuano ya kombe la dunia, mfungaji – miaka 17 na siku 239 (Brazil v Wales 1958)
5.Mfungaji wa hat trick mdogo zaidi katika World Cup – miaka 17 na siku 244 (Brazil v France 1958)
6.Mfungaji mdogo zaidi katika mchezo wa fainali ya Kombe la dunia  na mshindi wa taji hilo – miaka 17 na siku 249.
7.Lakini pia kama hufahamu tu ni kwamba Pele ndio mchezaji aliyeipa umaarufu style ya aina ya Bycle Kick baada ya kufunga bao kwa style hiyo.
8.Waldemar De Brito ni mchezaji wa zamani wa Santos na ndiye aliyempeleka Pele kucheza soka na siku aliyompeleka alimuambia kocha kwamba “huyu kijana atakuwa bora duniani”
9.Kwa kutambua mchango wa Pele, mwaka 1995 serikali ya Brazil ilimpa uwaziri wa michezo, alidumu katika cheo hicho hadi 1998.
10.Katika klabu ya Santos kila tarehe 19 November wanasheherekea Pele Day ambapo ndiyo siku ambayo Pele alifunga bao lake la 1000.
11.Baada ya Pele kustaafu, balozi wa Marekani nchini Brazil alinukuliwa akisema “kwa miaka 22 aliyocheza soka ameeneza amani na upendo kuliko ubalozi wowote ule duniani”
12.Muandishi mmoja wa vitabu Uingereza aliulizwa kuhusu tofauti ya Pele na wachezaji wengine akiwemo Di Stefanio na alijibu “Di Stefanio amezaliwa lakini Pele ametengenezewa mbinguni”
13.Jina la Pele ilikuwa nickname yake shuleni lakini familia yake ilimtambua kwa nickname ya Dico.
14.Pamoja na umahiri wake wote lakini Pele hajawahi kuvunja rekodi ya baba yake, baba mzazi wa Pele ameshawahi kufunga mabao 5 ya vichwa katika mchezo mmoja huku Pele magoli mengi ya vichwa katika mechi 1 ni manne.
15.Wazazi wake Dondinho na Celeste walimpa jina la Edson Arantes do Nascimento – ulimwengu wa soka unamtumbua kama #PELE – siku kama ya leo, Oktoba mwaka 1977 Pele alistaafu kucheza soka akiwa na klabu ya Cosmos ya nchini Marekani.

No comments