Header Ads

Video yahatarisha penzi la Cardi B na Offset


Rapa wa kike kutoka Marekani, Cardi B ameonesha kukasirishwa na kitendo cha mpenzi wake Offset kurekodiwa video na mwanamke mmoja maarufu nchini Afrika Kusini wakiwa kwenye pozi la mitego ya kimahaba.
Cardi B ametumia mtandao wa Instagram kueleza hisia zake kwa kutoa posti zenye utata nyingi zikimuonesha akitaka kurudia maisha yake ya zamani na kutemana na rapa Offset.
Video hiyo ya Offset na Mwanamke huyo iliwekwa kwenye mtandao wa Twitter na mdau mmoja kutoka Afrika kusini ikimuonesha Offset akiwa na mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Faith Nketsi na kumtag Cardi B kwa kuandika “Sis how do you feel about this @iamcardib?.
Baada ya kuona video hiyo Cardi B alianza kutoa posti kwenye ukurasa wake wa Instagram akionesha kukasirishwa na kitendo hicho kwa kuweka picha zilizoambatana na ujumbe wenye utata.
Hata hivyo, watu wengi wanaamini kuwa Cardi B huenda akaachana kabisa na Offset na kurudiana na mpenzi wake wa zamani ambaye ametoka gerezani siku chache zilizopita.
Rapa Offset alikuwa nchini Afrika Kusini na kundi lake la Migos Alhamisi hii kwenye ziara ya kimuziki na ndio huko walikokutana na mwanamke huyo ..

No comments