Header Ads

UWOYA ACHOSHWA NA DOGO JANJA


Dogo Janja.
MKALI kunako soko la filamu Bongo, Irene Uwoya, amesema kuwa amechoshwa kuuliza maswali juu ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’.
Akipiga stori Over Ze Weekend, Uwoya alisema kuwa suala la kuwa kwenye uhusiano kwake ni binafsi na haijalishi yupo na nani lakini pia hataki kusikia wala kuulizwa swali kuhusu msanii huyo.
Irene Uwoya.
“Sihitaji kumzungumzia (Dogo Janja) na nimechoshwa na maswali kuhusu kuwa kwenye uhusiano naye, hayo ni mambo yangu binafsi na ninaomba niachwe kwa kweli,” aliwaka Uwoya.

No comments