Header Ads

ROMA: KUTEMBEA NA WALETI NI MZIGO


Roma Mkatoliki.
STAA wa Ngoma ya Zimbabwe, Ibrahim Musa, ‘Roma Mkatoliki’ amefunguka kuwa, katika maisha yake kamwe hawezi kutembea na waleti mfukoni kwa kuwa ni kujipa mizigo ya bure na pia ni ushamba.
Akipiga stori na Over Ze Weekend, Roma alisema yuko tofauti na wanaume wengine wengi ambao hupenda kutembea na waleti kwa ajili ya kuhifadhia pesa, kwa upande wake anaamini ni kujipa mizigo isiyokuwa na sababu za msingi.
“Siwezi kujipa mizigo ya kubeba waleti muda wote, kama ni fedha huwa natunza kwenye mifuko ya suruali zangu, sijazoea kubeba waleti kwanza naweza kuidondosha,” alisema Roma.

No comments