Header Ads

Tukio la ubaguzi wa rangi laiponza Lazio, yafungiwa milango


Stadio Olimpico Curva ni kati ya viwanja ambavyo sio rafiki sana kwa wachezaji weusi, ni uwanja ambao umetawaliwa sana na mambo ya kibaguzi ambapo mashabiki wa Lazio hupatumia kuwashambulia watu weusi.
Claud Adpajong sio Muafrika ni Muitalia mwenye asili ya Ghana lakini pamoja na kuwa raia wa Italia ila rangi yake nyeusi ilimponza na kuzomewa vibaya sana wakati timu yake ya Sossulo ikifa bao 6 kutoka kwa Lazio.
Adpajong amesema alikuwa akisikia kelelel nyingi kila mara alipokuwa akiugusa mpira lakini hakupenda kuzifuatilia sana huku akishangazwa kwamba kuna watu hadi hii 2017 wanafanya mambo kama hayo.
Baada ya tukio hilo sasa chama cha soka nchini Italia kimekuja na adhabu kwa Lazio na itawalazimu kucheza michezo yao miwili huku milango ya uwanja ikiwa imefungwa(bila mashabiki).
Kwanza watakapoikaribisha Cagliari tarehe 22 na pia  watakapoikaribisha Udinesse November 5 michezo yote hii miwili itachezwa bila mashabiki kuwepo uwanjani.
Lazio ni kati ya vilabu ambavyo vinafanya sana matukio ya ubaguzi wa rangi kwani kama unakumbuka Antonio Rudiger wakati yuko Serie A alifanyiwa vitendo vya namna hii na mashabiki wa Lazio pamoja na kiungo wao Senad Lulic.

No comments