Header Ads

Nani kwenda kombe la Dunia kutoka Group C la Afrika?



Kueleka kwenye Mechi za Kufuzu kombe la Dunia kwa nchi za Afrika Shaffihdauda.com inatazama uso kwa uso timu zilizo katika Makundi yanayochuana kuwania nafasi hizo na leo tutaanza kwa kutazama Kundi C
Timu zilizopo kwenye Kundi hili ni
Mali
Gabon
Ivory Cost
Morocco
Mechi zitakazochezwa wiki Hii
Ijumaa Oktoba 6
Mali Vs Ivory Cost 
Uwanja – Stade Du 26 Mars-Bamako
Jumamosi Oktoba 7
Morocco Vs Gabon 
Uwanja – Stade Mohamed V Morocco
Mali Vs Ivory Cost 
Timu hizi mbili za Afrika Magharibi zimekutana jumla mara 25 kwenye michezo mbalimbali ya mashindano na kujipima nguvu, Ivory Cost wakiwa wameshinda jumla ya Michezo 16 Mali wakishinda 2 na wakitoka sare mara 7  Ivory Cost wakiwa wamefunga jumla ya magoli 47 katika mechi zao dhidi ya Mali ambao wameshinda jumla ya Magoli 17 na Mara ya mwisho wamekutana October 8 2016  ambako Ivory Cost Walishinda 3-1
Morocco Vs Gabon
Wakiwa wamekutana mara 14 huku Morocco wakiwa wameshinda jumla ya mechi 6 na Gabon kushinda 5 na kutoka sare mara 3 Morocco wakiwa wamefunga magoli 21 na Gabon kupata Magoli 12  mara zote waluzokutana huku mara mwisho kukutana ilikuwa ni October 8 2016 walitoka suluhu ya bila ya kufungana Morocco akiwa amecheza Mara nne michuano ya kombe la Dunia huku Gabon akiwa hajawahi Kushiriki Michuano hiyo.

No comments