Header Ads

STAR ZEAL AMEDROPISHA LIST YA WASANII (10) BONGO NA WATANO(5) KUTOKA TANGA ANAO WAELEWA ZAIDI



Msanii wa bongo fleva STAR ZEAL na hit maker wa ngoma ya BONGO MAN anaekuja kwa kasi zaidi kwenye indury ya burudani kutokea jiji la mahaba (TANGA) leo amepiga story na Hamisihemedi.com na kufunguka list ya wasanii anaowakubali zaidi kwenye mziki wa bongo fleva kutokea hapahapa kitaa cha 255 Bongo Tanzania.

Lakini kama nimfuatiliaji wa muziki wa kitanga tanga zaidi huenda ukabashiri list ambayo huenda Star zeal anaikubali zaidi kutokana na post zake ambazo huwa anapost kwenye mitandao ya kijamii huku akionesha baadhi ya vitu ambayo anajifananisha na mastaa wakubwa.
Na list ya star zeal ni kama ifuatavyo


1. DIAMOND PLATNUMZ


Kwanza kabisa namuelewa kazi zake lakini pia ni daraja la mafanikio kwa vijana kwa kuwa ametoa ajira zaidi ya 55, kingine diamond ni mtu ambae ana haso sana kuufikisha mziki wake katika level za kimataifa ameweza kutuwakilisha vizuri katika martaifa mengine.


2. ALLY SALEHE KIBA (KING KIBA)



Namkubali sana ALLY KIBA kwa kuwa ni msanii ambae anafanya vizuri kwa sasa na ngoma yake ya SEDUCE ME Lakini pia msanii ambae anapenda kukaa kimya ili mashabaiki wa mmisi kwenye game na akiachia ngoma kweli huwa inakubalika na kukata kiu ya mashabiki vile vile anatuwakilisha vizuri kwenye mataifa mengine.


3. DARASA CMG



Darasa ni mwanangu anawakilisha kitaa flani hivi cha kiwalani DSM jamaa ni mbunifu, japo alikaa kimya kwa mda kama miaka miwili lakini alivyorudi amekuja na vitu tofauti mfano ukiangalia staili ya uandishi wake lakini pia hata biti zake zimekuwa ni za kitofauti.



4. ASLAY  ISIHAKA
Aslay isihaka ni moja kati ya madogo ambao niliwaoona kwa mbali sana tangu anaanza mziki , ni msanii  ambae anauwezo wake binafsi. Aaa nimeweza kumweka katika nafasi ya 4 kwa kuwa ukiambiwa utaje wasaniii wa 5 bongo akimwacha Aslay utakuwa umefeli ukizingatia ngoma zake zinapendwa sana na akina dada.


5.  RAY VANNY


Ray ni mwandishi mzuri ambae anajua sana jinsi ya kuandika lakini pia ray pia ni mtu ambae nimeweza kuona haso zake  hivyo ananipa changamoto na mimi niweze kufikia mahali alipo lakini tukumbuke kuwa ndani ya mwaka mmoja tangu aingie WCB rayvany ni msanii pekee alio beba tuzo kubwa ya BLACK ENTERTAIMENT TELEVISION (BET) Tuzo ambayo hakuna msanii yoyote bongo aliewahi chukua.



6. YOUNG KILLER MSODOKI

A boy  from mwanza  jamaa ametoka mwaka 2012 lakini kabla ya hapo mimi nilikuwa namjua fresh na mimi ni shabiki namba moja wa young killer kutokana na mistari yake anavyoiandika yaani nani ya mistari yake miwili lazima utacheka au ufikirie kwanini ameandika vile.



7.  NIKI WA PILI



Niki wapili ni jamaa anaewakilisha kundi la weusi kutoka jijijni Arusha mshikaji ni genious ana staili yake ya uandishi pia ni msanii wa kuigwa sana ukizingatia jamaa bado anasoma msanii mwenye elimu yake daaaaah anajua sana thux why nikamtupia namba 7.


8.NIKI MBISHI


Jamaa anawakilisha pande za Songea ni mshikaji ambae alinipokea nilivyofika Tamaduni music pia mshikaji ambae anaushauri mzuri pia ame ispire wasanii wengi sana wa hiphop
Nakumbuka siku tunakutana aliniambia nina kitu hivyo nikaze buti ili watu wengine wanione kama alivyoniona yeye.

9. FID Q


Jamaa nawakilisha pande za Mwanza ni mshikaji ambae yuko fresh sana kwenye uandishi pia mshikaji ambae anaushauri mzuri kuna mstari wake unasema ‘’UTAAMBULIA USHAURI UKIHITAJI MSAADA WA KIFEDHA’’ pia ni sanii ambae amekuwa na uwezo mkubwa sana yaani

katika mistari nane lazima kuna kuna mistari miwil ambayo ni kawaida lakini huwa inamchukua mda mtu kuielewa kwa haraka mpaka ukae afikirie.



10. ROMA





Namkubali roma kwanza ni brother  wangu ambae tunatoka sehemu moja lakini pia ni m bunifu vilele amekuwa ni mtetetzi wa wanyonge pia amekuwa akiwakilisha changamoto za wanachi kwa serikali.


Pia Star zeal hakusita kufunguka kuhusiana na wasanii anao wakubali zaidi kwenye game ya Tanga
Na kusema kuwa yeye ni miongoni mwa msanii anaejikubali zaidi na akatoa shavu kwa wasanii wanne (4) anao waelewa kwa sasa
1. CASSIM WA LOE
2.FADHILY UWEZO
3. RAP KID
4.RAI MC

Story na Prismatics

No comments