Header Ads

RYAN GIGGS AZITOLEA MACHO LECEISTER CITY NA EVERTON


Jagina wa Manchester United na Wales Ryan Giggs amesema anavutiwa na nafasi za kazi za umeneja katika klabu za Leicester na Everton zinazocheza Ligi Kuu England.
Klabu zote mbili hazina mameneja baada ya Leicester kumfuta kazi Craig Shakespeare wiki iliyopita.
Everton walimpiga kalamu Ronald Koeman Jumatatu.
Giggs alikuwa mkufunzi msaidizi wa Louis van Gaal uwanjani Old Trafford, na alisailiwa kwa kazi ya umeneja Swansea mwaka 2016.
Koeman afutwa kazi Everton
“Kwangu, hizi ni klabu ambazo zinaweza kunivutia,” Giggs, 43, ameambia Sky Sports.
“Nafikiri ukiangalia timu hizi mbili, Leicester walikuwa mabingwa misimu miwili iliyopita, Everton nao ni klabu nzuri na yenye historia nzuri.
“Hata hivyo, kuna wakufunzi wengi huko nje ambao pia watavutiwa na nafasi hizo.”
Giggs haaminiki kuwa miongoni mwa wanaopigiwa upatu kuchukua kazi ya umeneja Everton.
Leicester nao wanaonekana kuimarika chini ya kaimu meneja Michael Appleton ambapo walilaza Swansea 2-1 uwanjani Liberty Stadium.
Klabu moja ya ubashiri imeweka uwezekano wa Giggs kuwa meneja wa Chelsea kuwa 12/1, Chris Coleman naye nafasi yake 6/1 na Claude Puel ndiye anayepigiwa upatu zaidi katika 4/7.
Giggs hajajishirikisha katika soka ya kiwango cha juu tangu kufutwa kwa Van Gaal Mei 2016.
Aliondoka katika klabu hiyo Julai 2016 na akaanza mapumziko ingawa amekuwa akisisitiza kwamba anakusudia baadaye kurejea kuwa mkufunzi katika klabu kubwa.

No comments