Header Ads

Nilianza mziki tangu mwaka 2010 ''NANDY''

Mwanga wa mafanikio umekuwa mkubwa sana kwa mwanadada Nandy ambae kwa sasa anafanya vizuri sana na ngoma yake ya ''WASIKUDANGANYE'' iliyofanyika kwa mshikaji wetu Imma the boy.
Sasa leo kupitia Hamisihemedi.blogspot.com Nandy amefunguka na kusema kuwa wengi wanaona kama yeye ameanza game hivi karibuni kumbe sivyo ambavyo wanafikiria na kusema kuwa yeye alianza game tangu mwaka 2010 na alipitia kwa watu mbalimbali akiwemo Prince Dully sykes.

Pia bidashost Nandy ameiambia hamisihemedi.com kuwa watu wakae mkao wa kula maana mda wowote anaweza akaachia mzigo mpya.

Na hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye exclussive interview na HAMISIHEMEDI.COM
Kwanini uliamua kumtumia  Ben pol kuwa video king........... aaaa kwanza kabisa kwenye video yangu ya wasikudanganye mimi pamoja na director tulipendekeza tumtumie msanii mwenzetu na tukaamua kumtumia Ben pol kwa kuwa ni mtu anaejulikna lakini pia ni mtu anaependa sana commedy kwahiyo tukaona anafaa.

Na vipi kuhusiana na na story ambazo zimezagaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na mahusiano yako na Billnas ...........''Billnas ni mtu ambae tunafahamiana tangu kitambo lakini pia ni msanii ambae nakubali sana kazi zake xo sisi ni washkaji rtuu kawaida hakuna mahusiano yoyote zaidi ya kazi'' alisema nandy

Ngoma iliyomtambulisha nandy kwenye game ni ''ONE DAY'' baada ya hapo akadropisha ngoma yake ya ''nagusagusa'' na sasa anafanya poa na ngoma yake ya wasikudanganye.

Na Hamisi Hemedi




No comments