NAPOLI WAKUTANA NA EFFECT ZA GURDIOLA CHAMPIONS LEAGUE,JESUS NA STERLING WATHIBITISHA
Kocha Pep Gurdiola amezidi kuonyesha makali yake katika kutengeneza kikosi imara baada ya jana kuweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya kikosi cha Napoli, Hii imekuwa ni mara ya 4 kwa Manchester City kupangwa na timu kutoka Italia katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya.
Man city walipata ushindi wa kwanza dhidi ya timu kutoka Itali ilikuwa ni mwaka 2014/15 dhidi ya AS Roma,Baada ya hapo City walikutana na mabingwa wa kihistira kutoka Italia Juventus katika msimu wa2015/16 na kufungwa katika mechi zote,Sasa ushindi wa City waliopata dhidi ya Roma ndio ushindi pekee kwa timu ya Man city dhidi ya waitaliano katika mechi zilizopita.

Sasa ushindi wa jana dhidi ya Napoli umeifanya klabu hiyo City kutopoteza katika mechi 13 wakiwa nyumbani
Post a Comment