Header Ads

Mabao 7 ya Liverpool hii leo yavunja rekodi ya Manchester United na kuweka rekodi mpya, matokeo yote haya hapa


Hii leo ilikuwa mara ya kwanza kwa klabu ya Liverpool kufunga idadi ya mabao 5 katika mechi ya ugenini katika michuano ya Champions League, michezo yao 45 iliyopita ya Champioms League hawakuwahi kufanya hivyo.
Robert Firminho (4), Phellipe Coutinho (13) na Mohamed Salaah (19,40) waliufanya mchezo uende mapumziko huku Liverpool wakiongoza kwa mabao 4 kabla ya Firmninho kuweka la tano kipindi cha pili.
Lakini bao la 6 la Oxlade Chamberlain liliwafanya kuwa klabu ya pili Uingereza kuwahi kufunga mabao 6 katika mchezo wa ugenini ya Champions League rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Manchester United huku ikiwa timu ya 9 kufanya hivyo.
Na bao la 7 la Alexander Arnold likawafanya Liverpool kuwa timu ya nne kuwahi kufunga jumla ya mabao 7 na zaidi ambapo timu za Bayern Munich, Barcelona na Lyon zimewahi kufanya hivyo na isitoshe kwa usiku wa leo Liverpool ilikuwa timu pekee ambayo haikuruhusu bao.
Manchester City waliipiga Napoli bao 2 huku Gabriel Jesus akifunga moja ya bao linalomfanya kufunga mabao 15 ndani ya michezo 22 ikiwa ni mchezo mmoja nyuma ya Kun Aguero wakati anafunga mabao kama hayo alipofika Man City.
Real Madrid wakiwa Santiago Bernabeu almanusra waambulie kichapo baada ya bao la kujifunga la Rafael Varane lakini dakika ya 43 ya mchezo Cristiano Ronaldo aliwaokoa Madrid kwa mkwaju wa penati.
Kwa suluhu ya leo Tottenham Hotspur wanakuwa timu ya tatu kuwahi kupata alama katika uwanja wa Santiago Bernabeu katika michezo ya Madrid 24 iliyopita katika Champions League.
Bao la Papstathopoulos liliookoa Dortmund kutoka katika kipigo na kuwafanya kutoka sare ya moja kwa moja dhidi ya Apoel Nicosia, huku Monaco wakifungwa 2 kwa 1 na Bestikas katika uwanja wao wa nyumbani.
Sevilla walijikuta wakiaibika kwa bao 5 kwa 1 kutoka kwa Spartak Moscow huku mabao ya Moscow yakiwekwa kimiani na Luiz Adriano, Promez, Giushakov na Dzhkiya.

No comments