Header Ads

NAILATY: MOBETO TULIA UWALEE WATOTO, ACHANA NA DRAMA


Hamisa Mobeto
MWANADADA anayefanya poa kwenye ulimwengu wa mitindo Bongo, Nailaty John ‘Nai Model’ amemfungukia mwanamitindo mwenzake, Hamisa Mobeto na kumtaka aachane na drama zinazozidi kupamba moto kila kukicha, kati yake na msanii wa Bongo Fleva aliyezaa naye.
Nailaty John ‘Nai Model’.
Akipiga stori na Za Motomoto News, Nai Model ambaye amewahi kufanya kazi ya kutangaza mavazi na mwanamitindo wa kimataifa, Flaviana Matata akitokea Talented Modeling Agency ya jijini Dar, amesema anachokifanya Mobeto, kuendelea kuvutana na baba wa mtoto wake, ni sawa na kuendelea kumwagia petroli kwenye moto kwani atakayeathirika zaidi ni mtoto waliyezaa naye.

“Mobeto ni dada yangu na mwanamitindo mwenzangu, najua anaumizwa na kinachoendelea ila nachomshauri, akae na kutulia awalee watoto, aachane na drama za kwenye mitandao ya kijamii kwani zinazidi kumharibia ‘image’ yake na tasnia nzima ya modeling,” alisema Nai Model ambaye anatarajiwa kuuza nyago kwenye video mpya ya msanii aliyetokea Yamoto Band, Beka

No comments