Gigy Money adai Hemedy PhD siyo level zake, ‘hana hela’
Video Vixen Bongo aliyeamua kutumbukia katika muziki, Gigy Money amedai msanii Hemedy PhD siyo level zake kwa sababu hana fedha.
Kauli ya Gigy Money inakuja baada ya hapo awali kuripotiwa kupishana kauli kwa wawili hao na Hemedy alipoulizwa na kipindi cha The Playlist cha Times Fm alijibu hawezi kumzungumzia Gigy.
Gigy akipiga stori na Bongo5 amesema kuwa yeye kwanza hamjui Hemedy na hana hadhi ya kuongea na yeye. “Hawezi kuwa na hadhi ya kuniogelea mtu kama mimi kwa sababu hana hela”, amesema.
Hemedy na Gigy wote wanajihusisha na ‘vitu’ viwili katika tasnia ya burudani Bongo, Gigy anafanya muziki na video vixen, Hemedy muziki na uigizaji.
Post a Comment