Header Ads

LIVE KUTOKA UWANJA WA UHURU: SIMBA 1-1 MTIBWA SUGAR (FULL TIME)


MPIRA UMEKWISHAAAA
GOOOOOOOOOOOOOO Dk 90+3 Okwi anaisawazishia Okwi kwa mpira wa adhabu, anaachia mkwaju mkali unaomshinda unaomshinda kipa Tinocco
SUB anatoka Kihimbwa, anaingia Henry Joseph upande wa Mtibwa

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 89 Sabato anaingia vizuri tena, anatoa na kuwa konaaa, inachongwa na kuwa goal kick
Dk 87 kona safi kabisa lakini Manula anaruka vizuri na kudaka
Dk 86 Kihimbwa anaingia tena ndani, anaachia shuti hapa, Manula anaokoa vizuri na kuwa kona


Dk 86 Mohamed Issa anaachia mkwaju mkali hapa, goal kick
Dk 84 hatari katika lango la Simba hapa, Dilunga anaingia na kuachia mkwaju mkali hapa...goal kick
Dk 83 Ndemla anaachia mkwaju mkali hapa, kama kawaida anapaishaa juu 
Dk ya 80, zimebaki dakika 10 tu na inaonekana wazi Simba presha inazidi kupanda
Dk 78, Dakika zinazidi kuyoyoma na Simba wanaonekana wanazidi kuwa na presha
Dk 77, mpira wa kona unaingia vizuri kabisa lakini Okwi anaukosa
Dk 76, Nyoni anaingia vizuri kabisa lakini Mtibwa Sugar wamejipanga vizuri
Dk 72 Dilunga anaachia shuti hapa hapa lakini nyanya kwa Manula
SUB Dk 69 Salum Hamis anakwenda nje upande wa Mtibwa Sugar na nafasi yake inachukuliwa na Hassan Dilunga
Dk 67, Pasi ya Nyoni, Ndemla anaachia mkwaju mkali hapa lakini goal kick


SUB Dk 64 Kichuya anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Said Ndemla
Dk 60, Okwi anaachia mkwaju mkali lakini anamlenga kipa
SUB Dk 57 Kelvin Kongwe Sabato anaingia kuchukua nafasi ya Mbonde ambaye ameumia
Dk 55, Okwi anaingia vizuri ndani ya 18 lakini shuti lake halikulenga lango
Dk 51, basi nzuri sana ya Mohamed Issa lakini Stamili Mbonde anaikosa kidogo tu na kuanguka mwenyewe. Yuko chini anatibiwa
SUB Dk 49 Mbode anatoka kwa upande wa Simba na nafasi yake inachukuliwa na Mganda, Juuko Murshid
Dk 45 Kipindi kimeanza na inaonekaan Simba wanataka kusawazisha lakini Mtibwa wanataka kuongeza bao la pili

MAPUMZIKO

DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 44, Niyonzima anaachia mkwaju wa faulo lakini unakuwa nyanya kabisa kwa kipa
Dk 42 Nyoni anacheza kona nyingine nzuri kabisa hapa, lakini safari Mtibwa Sugar wanaokoa vizuri kabisa
Dk 41, Kotei anaachia mkwaju inakuwa kona, inachongwa wanaokoa tena inakuwa kona
Dk 38, Simba wanaingia vizuri lakini shuti kali la Okwi linapaa juuu 
GOOOOOOOOOO Dk 36, kona safi, mabeki wa Simba wakiwa wmazubaa, Mbonde anaruka na kufunga kwa kichwa
Dk 35, Mtibwa wanachonga kona, shuti Manula anatema inakuwa kona tena


Dk 35, Kihimbwa anaingia vizuri tena, inakuwa konaDk 30, Simba wanaingia vizuri tena, Okwi anajaribu inakuwa kona
Dk 27, Kanoni anaachia mkwaju wa faulo ya adhabu lakini goal kick
Dk 23, Liuzio nje ya 18 anaachia mkwaju lakini unapita juu, goal kick
Dk 21, Kotei anageuka na kuachia mkwaju mkali, unamgonga beki na kuwa kona
Dk 19 Kihimbwa wa Mtibwa anampita Shomari kwa mara ya pili na kuachia krosi safi kabisa
SUB Dk 17 Juma Liuzio anaingia kuchukua nafasi ya Bocco aliyeumia
Dk 16, krosi ya Okwi inaokolewa na kuwa kona. Inachongwa, Niyonzima anapiga shuti, goal kick
Dk 14, Mtibwa wanafanya shambulizi zuri hapa lakini wanashindwa kumalizia


Dk 12, Bocco yuko chini pale, inaonekana kama alipata dhoruba
Dk 9 Bocco alikuwa ameingia vizuri lakini beki amemkamata na mwamuzi kaweka faulo 
Dk 5, Simba wanapata kona baada Okwi kuzuiwa na mpira kwenda nje
Dk 2 Manula analazimika kuruka juu kuokoa mpira wa faulo, anaanguka na kulalamika maumivu lakini ameamka
Dk 1, Simba wanaonekana kuanza kwa kasi wakitaka kupata bao la mapema. Wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Mtibwa lakini mpira hauna madhara

No comments