Header Ads

Lebron James Apigania Usawa Wa Weusi Kwa Weupe Kwa Staili Yake.


Ligi kuu ya NBA ya nchini Marekani, ilianza mzunguko wake mpya tarehe 17 Oktoba na huu ni msimu wa 72 wa ligi hii ambapo mchezo wa kwanza ulihusisha vilabu vya  Cleveland Cavaliers na Boston Celticskatika uwanja wa nyumbani wa Cavs’ unaofahamika kama Quicken Loans Arena. Tofauti na ligi za michezo mingine, hapakuwepo na matukio yoyote makubwa yaliyohusisha kwenda kinyume au kupinga wimbo wa Taifa ikiwa kama ishara ya kupigania umoja na mshikamano nchini Marekani.
Wachezaji wa Cavs wao walishikana mikono kama ilivyokuwa katika hatua ya michezo ya maandalizi huku Celtics wao wakisimama wima kama timu moja, wakifuatana kwa usawa wa mabega huku wachezaji kadhaa na makocha wakiwa wameweka mikono yao kifuani kipindi ambacho kamanda wa jeshi mstaafu, Generald Wilson alipowaongoza kuimba wimbo wa Taifa.
Hata hivyo baada ya taa kurejea na mwanga kutawala katika uwanja wa  Quicken Loans Arena, nyota wa Cavs  LeBron James aliacha miguu yake izungumze badala ya kinywa chake.
Lebron James alivaa viatu ikiwa ni staili mpya vinavyofahamika kama Lebron 15 vikiwa na maandishi yanayong’ara kwa nyuma yakiwa yameandikwa EQUALITY. Viatu vilikuwa vyeusi isipokuwa maneno hayo yenye maana ya USAWA yakiwa katika rangi inayong’ara ya dhahabu.
Wakati watu wote wakitizama namna ambavyo migomo ikiendelea kwenye ligi ya NFL ambayo inasimamia mchezo wa American Football, James aliamua kuwa kwenye siku ya ufunguzi angefanya kitu ambacho kingeweza kusaidia namna ya kuongeza uelewa wa yote yanayoendelea kuhusiana na watu weusi dhidi ya weupe wa Marekani.
“Nilitaka kufanya hili jambo liendelee kuzungumzwa katika hali chanya, liendelee kupigiwa kelele,,” James alikiambia kituo cha  ESPN baada ya timu yake ya Cavs’ kupata ushindi wa 102-99. “Tunafahamu ugumu tunaoupitia, tunafahamu tuliyopitia kama Taifa na kama dunia kwa ujumla. Hivyo nilipata nafasi ya kutumia jukwaa na fursa yangu na nikafanya hivyo.”
Nike, ambayo Lebron amesaini nao mkataba wa Maisha, walianzisha kampeni ya USAWA unayoweza kuisoma hapa (EQUALITY campaign) mwezi  February wakiwa na lengo la kutumia wachezaji wao kupaza sauti kwa kutumia nguvu ya michezo kuwataka watu kusimamia haki na usawa kwenye jamii walizomo.
Viatu alivyoviaa James havitouzwa na vyanzo mbalimbali vikiripoti kuwa hii itakuwa ni kwa ajili ya wachezaji pekee. Hata hivyo katika sehemu ya kampeni hii kutakuwa na kiwango cha dola milioni 5 zitakazotolewa na NIKE kwa mashirika mbalimbali ambayo yanasimamia na kusisitiza Amani, ambayo yanajenga mahusiano ya watu ndani ya jamii.

No comments