La Liga waendelea kukomalia pesa za PSG, waipa UEFA msimu mmoja kuwatimua laa sivyo watakwenda mbali zaidi
Shirikisho la soka nchini Hispania La Liga liliwahi kulikataa dau ambalo PSG walilitoa wakati wa usajili wa mshambuliaji wa Barcelona Neymar wakisisitiza kwamba kiasi hicho cha pesa ni kikubwa kuliko uwekezaji wa PSG.
La Liga walikuwa wakiamini kwamba klabu ya PSG unakiuka sheria za kuhusu matumiza ya usajili za Financial Fair Play, kitendo ambacho PSG walikana na maisha yakaendelea huku Neymar akianza kukipiga PSG.
Wakati watu wakiamini kwamba hoja ya La Liga kuhusu PSG imekwisha sasa raisi wa La Liga Javier Tebas ameibuka tena na kudai kwamba miamba hiyo ya Ufaransa inafanya mchezo mchafu kuhusu uchumi.
Sheria za matumizi ya FIFA zinaziruhusu timu kufanya manunuzi na matumizi kutokana na pesa wanayoipata tu katika uwekezaji wa soka huku PSG ikidaiwa kupata msaada wa serikali ya Quatar kufanya matanuzi katika soka.
Javier Tebas amehoji uwezo wa kifedha wanaounesha PSG unatokea wapi, na nguvu yao kuwa kubwa kama Manchester United, Real Madrid na Barcelona wanaitoa wapi kama sio pesa ya nje ya soka?
Tebas amesema uhusiano uliopo kati ya PSG na kampuni ya michezo ya QSI ya Quatar inawasaidia PSG kuingiza pesa kutoka vyanzo vya nje ya soka na amesema njia hiyo hiyo ndiyo inatumiwa na Manchester City.
Mapato tu yanayopatikana kutokana na masuala ya matangazo ya Tv yanaonesha PSG wanaingiza kiasi kidogo sana tofauti na pesa wanazotumia kwani wanaingiza euro 43m huku klabu kama Real Madrid wanaingiza euro 121m.
Tebas amesema suala wanalofanya PSG linaathiri soka moja kwa moja na kuwataka UEFA kuanza kulichukulia kwa uzito mkubwa suala hilo kwani vilabu vingine vinaathirika sana na matumizi hayo.
Tebas ameonya kwamba kama UEFA watashindwa kuchukua hatua hadi mwisho wa msimu huu watakwenda ngazi za juu zaidi na kama wakipatikana na hatia baasi wafukuzwe katika michuano ya Champions League.
Post a Comment