KIMENUKA Mitandaoni! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema, kufuatia sakata la mshindi wa Big Brother Africa ‘BBA’ mwaka 2014, Idris Sultan, ambaye kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, aliandika ujumbe kwa mzazi mwenziye mwanamitindo, Hamisa Mobeto, wa kumshauri kuhusiana na Rav 4 aliyomzawadia mwanamitindohuyo, pamoja na gharama za matumizi.
MOBETO AJIBU!
Baada ya ujumbe huo, nyongoikamtibuka Mobeto, na kuamua kurudisha majibu kwa Idris.
IDRIS AOMBA MSAMAHA
Mara tu baada ya kuona kuwa Mobetoamekasirika, Idris akapost tena ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram, na kumuomba msamahamwanamitindo huyo, huku akijitetea kuwa hakumaanisha alichokisema, ulikuwa ni utani tu.