Header Ads

Kipigo cha Chelsea vs AS Roma kilichomuwekea rekodi Stephan El Shaarawy



Usiku wa October 31 2017 michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya maarufu kamaUEFA Champions League iliendelea kwa michezo nane kuchezwa barani Ulaya, Barcelona walikuwa ugenini kucheza dhidi ya Olympiakos game ambayo imemalizika kwa sare tasa.
Chelsea walikuwa Italia kucheza dhidi ya wenyeji wao As Roma na kujikuta wanakubali kipigo cha magoli 3-0 wakati Manchester United walikuwa nyumbani Old Trafford kucheza dhidi Benfica ya Ureno game ambayo imemalizika kwa Man United kupata ushindi wa magoli 2-0.
Game ya Chelsea dhidi ya AS Roma ndiogame ambayo ilikuwa inatajwa kuwa itavuta hisia za mashabiki wengi kutokana na Chelsea na Roma zote zipo katika kiwango kizuri na katika msimamo wa Kundi C zilikuwa zinafukuzana.
Chelsea wamekubali kipigo cha magoli 3-0 dhidi ya AS Roma magoli ya Romayakifungwa na Stephen El Shaarawyaliyefunga magoli mawili dakika ya 1 na dakika ya 34.
Msimamo wa Kundi C ulivyo kwa sasa
Magoli hayo yamemfanya Stephen El Shaarawy kuweka rekodi ya kufunga magoli mawili katika game moja ya UEFA Champions League kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya soka na baadae Diego Perotti akafunga goli la tatu dakika ya 63.
Matokeo ya game nane za UEFA Champions League zilizochezwa usiku wa October 31 2017.

No comments