FIFA waanza kufikiria kufanya mabadiliko kwenye suala la uraia wa wachezaji
Shirikisho la soka duniani FIFA linafikiria kubadilisha sheria zinazoongoza uhalali wa mchezaji kuitumikia timu ya taifa aitakayo.
Kwa sheria zilizopo sasa, wachezaji ambao wameshacheza mechi za mashindano rasmi wakiwa na timu fulani ya taifa basi wanakosa uhalali wa kutumikia taifa lingine endapo watahitaji kufanya hivyo
Shirikisho la soka la Cape Verde limetoa wazo la sheria hii kupunguzwa makali endapo mchezaji husika atakuwa amecheza mechi 1 au 2 kwa timu fulani ya taifa basi aruhusiwe kufanya mabadiliko kama atakuwa amekidhi vigezo vingine.
“Dunia inabadilika, masuala ya uhamiaji pia ynabadilika. Kuna masuala ya uraia ya uraia yameanza kuibuka duniani kote – upande wa Africa, Asia na upande wa Concacaf kuna matatizo mengi yanayohusu uraia wa wachezaji.
“Hivyo ni muda mzuri wa kuangalia upya sheria zetu na kuona kama kutakuwa na suluhisho zuri ambalo halitokuwa na shida kuuboresha zaidi mchezo wetu wa soka.” – Victor Montagliani, mjumbe wa kamati kuu ya FIFA na Rais wa CONCACAF.
Sheria nyingine ya FIFA inaelekeza kwamba mchezaji ambaye hana uhusiano wa damu na nchi husika ataruhusiwa kuitumikia nchi hiyo endapo tu ameishi na kucheza soka ndani hiyo nchi kwa miaka 5.
Montagliani anasema Kamati Kuu ya FIFA inafikiria mabadiliko ya kanuni na sheria inayohusu jambo hilo, huenda wakapunguza muda au kuongeza pia.
Pia aliongeza kwamba FIFA inaweza kuangalia suala la fidia katika kesi ambazo mchezaji anakuwa amefundishwa na kukuzwa kisoka na nchi nyingine akiwa kinda halafu baadae akaenda kulitumikia taifa lingine.
Mwaka 2004, Antar Yahia alitengeneza historia wakati alipokuwa mchezaji wa kwanza kuitumikia timu ya taifa katika ngazi ya juu wakati alishawahi kuitumikia timu ya taifa linginr kstika ngazi ya chini.
Yahia, ambaye alikuja kuisadia Algeria kufuzu kucheza kombe la dunia 2010, alishawahi kuitumikia Ufaransa U18 wakati akiwa mdogo.
Huko nyuma, mchezaji ambaye alishawahi kuitumikia nchi moja katika mechi ya mashindano rasmi katika kikosi cha wakubwa au makinda, basi hakuwa na uhalali tena wa kwenda kubadili raia na kutumikia taifa lingine.
Post a Comment