Header Ads

Kilichojiri mahakamani jana katika kesi ya Lukaku


Wakati wa mapumziko ya ligi mbali mbali barani Ulaya miezi michache iliyopita klabu ya Mancehseter United walikuwa nchini Marekani kujiandaa na msimu huu wa ligi, United walikuwa hapo kabla hata hawajamnunua Romelu Lukaku.
Lukaku alipokuwa Marekani siku chache kabla ya kusaini United lakini wakati akiwa Marekani mshambuliaji huyo alijikuta matatizoni na polisi baada ya kukamatwa akifanya party nyumba aliyofikia huku akiweka sauti kubwa ya mziki.
Lukaku alifunguliwa kesi mjini Los Angels lakini kesi hiyo iliahirishwa ikisubiri tarehe nyingine ya kusomwa na hii leo mahakama jijini Los Angels imesoma kesi hiyo na kumtajia Lukaku makosa yake.
Lukaku hakuwepo mahakamani lakini wakili wake aitwaye Robert Humphreys alikuwepo mahakamani kumuwakilisha lakini akakana makosa yote yamhusuyo Lukaku.
Jaji wa kesi hiyo amemtaka Lukaku kufika tena mahakamani hapo November 21 na anaweza kupigwa faini kubwa pamoja na kulipia gharama ambazo polisi waliingia wakati wa kwenda kulichunguza tukio hilo.

No comments