Joh Makini.
MKALI wa Muziki wa Hip HopJoh Makini pamoja na mkali wa miondoko ya Zouk Rhumba, Barnaba wanatarajiwa kuongoza wakali 25 ndani ya Uwanja wa Taifa wa BurudaniDar Live uliopoMbagala – Zakhem jijini Dar.
Akizun-gumza na Risasi Vibes, Meneja na Mratibu wa Dar Live, Rajabu Mteta ‘KP Mjomba’ alisema kuwa usiku huo utatambulika kamaFuniko Concert likijumuisha wakali kibao katika Muziki wa Hip Hop, Zouk pamoja na Singeli.
Barnaba.
“Utakuwa ni usiku wa kihistoria tangu Dar Live ianze, mashabiki kwa mara ya kwanza wategemee kuwaona wakali zaidi ya 25 ambao baadhi yao ni Billnas, Barakah The Prince, Moni, Man Fongo, Amber Lulu, Baucha, Pam D, Linex, Jay Moe na Mesen Selekta huku MC akiwaMr. T Touch na Meneja Maneno,alisema KP. Funiko Concert imedhanimiwa na Global Groupkupitia Dar Live.