Header Ads

Antonio Conte kutimuliwa Chelsea? Wengine hawa hapa


Uwekezaji unaofanywa na timu za barani Ulaya haswa Uingereza unawafanya mabosi kukosa uvumilivu kwa makocha wao, miezi mitatu tu tayari Craig Shakespaere, Ronald Koeman na Frank De Boer wametimuliwa lakini nani amafuatia?
Antonio Conte? Ni kocha ambaye ana presha kubwa sana kwa sasa, aliwapa Chelsea ubingwa msimu uliopita lakini matokeo ya siku za hivi karibuni ya Chelsea yanaweza kumtibua tajiri Abromovich.
Katika michezo minne ya Chelsea iliyopita wameshinda mchezo mmoja tu na hiyo inazidisha presha darajani huku tetesi kutoka klabuni hapo zinasema kuna msuguano wa chinichini kati ya Conte na viongozi wa timu.
Slaven Bilic, sasa achana na Conte ,kocha wa West Ham Slaven Bilic anaonekana wazi kwamba anaweza kuondoka wakati wowote kuanzia sasa kutokana na ubovu wa West Ham msimu huu.
Hawana matokeo mazuri hata kidogo katika Epl lakini kipigo cha bao 3 kwa sifuri toka kwa Brighton Ijumaa iliyopita kinaweza kumuweka Bilic kwenye nafasi kubwa kufungashiwa virago.
Mark Hughes, Stoke City nao pamoja na mwenyekiti wa timu kumuunga mkono Hughes lakini uwepo wao katika nafasi ya 17 unatishia uhai wao katika Epl na ni wazi mabosi wa Stoke hawatakuwa tayari kuvumilia hilo.
Paul Clement, Clement na yeye ni kati ya wanaopewa nafasi kubwa kuondoka Epl, wameshapigwa mara 5 katika michezo 9 huku jana wakitolewa katika michezo ya Efl na wiki ijayo wako na Arsenal.
Maurcio Pellegrino, Southampton wamesuluhu mara tatu, wamepigwa mara tatu na kupata ushindi mara nne lakini mabosi hawaridhiki na maendeleo ya katika timu hiyo kwani hadi sasa wako nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi.

No comments