Belle 9 achokonoa jambo record label Bongo
Mkali wa muziki wa RnB Bongo, Belle 9 amefunguka mtindo wa record label Bongo kutambulisha wasanii wapya bila kufanya usahili wa wazi.
Hitmaker huyo wa ngoma Give It To Me na Ma-Ole ameiambia Dj Show ya Radio One kuwa kufanya hivyo ni ile kulinda ule upya wa msanii wala haina athari zozote.
“Wanafanya hivyo kwa ajili ya kutengeneza ule upya wa msanii ili wakija kutangaza ile siku wanamsaini msanii fulani anakuwa mpya, usahili unaweza ukafanya watu wakamtambua msanii, hivyo siku anatambulishwa anakuwa hana kitu kipya kwa watu,” amesema Belle 9.
Ameongeza kuwa kwa upande wake anaona kitendo cha kutofanya usahili siyo kibaya kwa sababu tayari kunakuwa na chachu ya mashabiki kutaka kujua uwezo wa msanii husika.
Post a Comment