Header Ads

BARCELONA YAAMUA KUVUNJA REKODI KUMBAKIZA MESSI, ITAMWAGA SH BILIONI 234.5


FC Barcelona imeamua kumbakiza kundini mshambuliaji wake nyota, Lionel Messi.

Ili kumbakiza, FC Barcelona imeamua kutoa kitita cha pauni milioni 80 (zaidi ya Sh bilioni 234.6) kumlipa Messi kama bonus ya usajili wake.

Kama Barcelona itafanya hivyo, itakuwa imeweka rekodi ya usajili kwa mchezaji ambaye tayari yuko ndani ya klabu kulipwa kitita kikubwa hivyo cha fedha wakati wa kuongeza mkataba.

Hata hivyo imeelezwa, FC Barcelona imelazimika kutafuta mdhamini ambaye ameipa fedha hizo na yenyewe italipa kwa kumtangaza.


Imeelezwa suela hilo la mdhamini litakuwa siri hadi hapo baadaye kila kitu kitakapomalizika.

Gazeti la kila wiki la nchini Hispania la L’Ara limeeleza kuwa klabu hiyo imeamua kufanya hivyo kuhakikisha Messi ambaye ni kama nembo ya klabu hiyo haondoki.

Moja ya timu zilizokuwa zimeanza kumfuatilia ni Manchester City inayofundishwa na kocha wake wa zamani, Pep Guardiola.

No comments