Header Ads

Baraka Afunguka Kuhusu Ugomvi na Alikiba


Msanii Baraka The Prince ambaye alikuwa chini ya lebo ya Rockstar4000 ambayo kwa sasa inaongozwa pia na msanii Alikiba, amesema hana tofauti yoyote na Alikiba licha ya kuondoka Rockstar4000.

Baraka The Prince ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba hajawahi kugombana na Alikiba, ingawa tangu atoke Rockstar4000 hajawahi kuwasiliana naye.
Baraka The Prince amendelea kwa kusema kwamba watu ndio wanaaminisha wenzao kwamba wawili hao wana tofauti, na licha ya kutoka Rockstar4000, bado hajaambiwa sababu rasmi ya yeye kuondolewa.

Tazama video yote hapa chini

No comments