Header Ads

Arsenal yakaribia kumilikiwa na mtu mmoja, wazee wapinga


Kwa muda sasa kumekuwa na majaribio ya chinichini kati ya wamiliki wakubwa wa hisa za klabu ya Arsenal kuhusu kujaribu kuinunua klabu hiyo, Alisher Usmananov na mmiliki mkuu wa hisa za klabu Stan Kroenke wamekuwa wakitunishiana misuli.
Mwezi wa tano mwaka huu Usmananov raia wa Urusi  alifanya jaribio la kuimiliki klabu ya Arsenal kwa kujaribu kumiliki hisa zote za klabu hiyo lakini jambo hilo halikuwezekana kutokana na kuwekea ngumu na Kroenke.
Sasa Stan Kroenke ambaye anamiliki 67% ya hisa za klabu ya Arsenal ameamua kutangaza ofa ya £528m ambapo kila hisa atainunua kwa £28,000 kiasi amabacho kinasemekana kinaweza kumvutia Usmananov.
Usmananov anamiliki 30% za klabu hiyo, lakini japokuwa Usmananov na Kroenke wamekuwa wamiliki wakubwa wa hisa katika klabu hiyo kwa muongo mmoja sasa lakini matajiri hao wawili hawana uelewano mzuri katika kazi.
Kama Kroenke atafanikiwa kununua hisa za Usmananov baasi atamiliki 97% ya hisa za Arsenal na huku 3% zinazobaki zikibaki kwa wamiliki wadogo wa Arsenal ambao wengi ni wazee wa kitambo wa klabu hiyo.
Umiliki wa 97% kwa Kroenke utakuwa umemuweka kwenye nafasi nzuri kujaribu kushawishi kuchukua hisa 3% zilizobakia na hali hii moja kwa moja itamfanya kuimiliki Arsenal na vitu vyake vyote.
Lakini wakati Kroenke anajaribu kununua hisa za Usmananov, wamiliki wadogo wa hisa za Arsenal ambao wengi wapo Arsenal kwa ajili ya mapenzi yao na klabu hiyo na sio faida ya kifedha kama ilivyo kwa Usmananov na Karoenke hawakubaliani na jaribio hilo.
Msemaji wao ameonesha hofu ya klabu kupelekwa itakavyo na mtu mmoja huku akihoji kama Karoenke anaona anaweza jukumu hilo mbona timu haifanyi vizuri? Lakini pamoja na yote hayo ni wazi Usmananov kuna asilimia kubwa atauza hisa zake.

No comments