Al Ahly waipa kipigo cha mbwa mwizi Etoile Du Sahel na kwenda fainali
Baada ya kushinda bao mbili kwa moja nchini Tunisia siku chache zilizopita, hii leo klabu ya Etoile Du Sahel hawakuamini kilichowatokea katika dimba la Al Ahly baada ya kupeea kipigo cha mbwa mwizi.
Al Ahly waliwaadhibu bila huruma Etoile Du Sahel kwa kuwapiga bao 6 kwa 1 na kipigo kilianza dakika ya kwanza tu kwa bao la Ali Maaloul kabla ya Walid Azorou kuweka kambani bao mbili kabla ya half time.
Kwa matokeo ya leo Al Ahly watakabiliana na Wydad Casablanca katika fainali ya michuano hiyo ya mabingwa wa Afrika, Wydad Casablanca walifudhu kwenda fainali baada ha hapo jana kuwafunga Usm Alger mabao 3 kwa 1.
Post a Comment