Header Ads

AC Milan na Inter Milan hawana mpango wa kutengana


Vilabu viwili vikongwe katika ligi ya mpira ya nchini Italia Ac Milan na Inter Milan wameungana katika suala la kuboresha kiwanja chao cha nyumbani cha San Siro ili kuonekana bora zaidi.
Wawakilishi wa vilabu hivyo walikutana na meya wa jiji la Milan Giussepe Sala ili kuongea juu ya utengenezaji huo mpya wa uwanja wao ambao unaingiza mashabiki 80,000.
Vilabu vyote viwili viko tayari kuchangia kifedha utengenezaji huo ambapo wanaona San Siro imekaa kizamani na kujaribu kuufanya kuonekana wa kisasa zaidi kwa kufanya marekebisho makubwa.
Makubaliano haya kati ya Ac Millan na Inter Milan yanafuta tetesi ambazo zilizagaa kwamba moja kati ya vilabu hivi viwili watahama uwanja huu siku za usoni, kwani hii inaonesha jinsi gani wote hawana mpango wa kuondoka San Siro.
Giussepe Sala amesifu mpango huo wa Ac Milan na Inter Milan na akasisitiza kwamba sio faida tu kwa vilabu hivyo viwili lakini uwepo wa uwanja bora utaongeza thamani ya jiji la Milan.

No comments