Header Ads

WENGER ANAAMINI SANCHEZ YUKO VIZURI KIAKILI, ILA KIMWILI...




Na Saleh Ally, London
Kocha Arsene Wenger amesema mshambilizi wake, Alexis Sanchez yuko vizuri kiakili lakini kinachotakiwa ni mazoezi awe fiti zaidi.

Sanchez alirejea mazoezini Arsenal Alhamisi ikiwa ni siku chache baada ya uhamisho wake wa pauni milioni 60 kwenda Man City kukwama.

Lakini kutoka hapa jijini London, Wenger akizungumza katika mkutano na waandishi wa habri katika eneo la Colney nje kidogo ya jiji la London amesema Sanchez anachotakiwa ni kufanya mazoezi ya kutosha ili awe fiti hasa.
“Ninaamini kiakili yuko vizuri kabisa tayari kwa kazi,” alisema Wenger.


Sanchez raia wa Chile alionyesha wazi kuwa alipania kuondoka Arsenal na kwenda Man City lakini mwishoni kabisa mambo yalikwenda tofauti.

No comments