WASANII WA BONGO FLEVA WATIFUANA NA WAFANYAKAZI WA KAMPUNI YA SIMU
Mgeni rasmi wa mechi hiyo Balozi wa Vijana Usalama Barabarani, James Mwakibinga akisalimiana na wachezaji wa timu zote mbili.
… akisalimiana na wachezaji wa timu ya Bongo Fleva.
Kikosi cha timu ya Bongo Fleva wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mpira kuanza.
Kikosi cha timu ya Airtel wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mpira kuanza.
Mwakibinga akizungumza na Global TV Online uwanjani hapo.
Mtanange ukiwa umeanza.
MTANANGE wa soka kati ya timu ya wasanii wa Bongo Fleva na wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano Airtel, umetimua vumbi katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers, Kawe jijini hapa kwa lengo la kudumisha umoja na mshikamano.
Katika mechi hiyo, mgeni rasmi alikuwa ni Balozi wa Vijana Usalama Barabarani, James Mwakibinga ambapo akizungumza kabla ya mchezo huo, aliwasifia wachezaji wa Bongo Fleva na wa Kampuni ya Mawasiliano Airtel kwa kuungana pamoja na kucheza mchezo wao wa kirafiki.
“Nawapongeza wote mliofika na kushiriki mchezo huu, ni jambo la busara kwenu kuwa wamoja na kudumisha amani ya nchi yetu.
“Katika kuhakikisha tunaunga juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, katika kuendeleza umoja baina ya mtu mmojammoja na hata makampuni kama ilivyotokea leo kwa Airtel na Bongo Fleva,” alisema Mwakibinga.
Post a Comment