SPORTPESA YATOA CHETI CHA SHUKRANI KWA JESHI LA POLISI, IGP SIRRO AFUNGUKA
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro ameipongeza Kampuni ya Michezo ya Kubashiri nchini, SportPesa ambayo imekabidhi pesa kiasi cha Tsh. Milioni 20 kwa Timu ya Mpira wa Miguu ya Jeshi la Polisi nchini, Polisi FC, katika hafla iliyofanyika kwenye Makao Makuu ya Polisi Dar.
“SportPesa ni wadau wetu na ni wadau welevu, wameona umhimu wa kuchangia fedha na vifaa vya michezo kwa Timu ya Polisi, hii itatusaidia sana.
“Naahidi kwamba fedha hizo tutazitumia vizuri kujiandaa kwa ajili kupanda na kuingia Ligi Kuu kwa moto mkali na kuhakikisha kuwa tunaleta heshima kwa Jeshi la Polisi na wafadhiri wetu mliotupatia vifaa vyetu leo,” alisema IGP Sirro.
Mbali na fedha hizo, SportPesa pia wamekabidhi vifaa vya michezo kwa klabu hiyo ili kuwawezesha kufanya mazoezi na na vingine watakavyotumia kwenye mechi mbalimbali za timu hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo, mkurugenzi wa utawala na utekelezaji Wa sportpesa, Tarimba alisema: “Tunatambua mchango wa timu ya polisi Tanzania kwa Jamii kiujumla kwani wanafanya kazi kubwa kuhakikisha sheria za nchi zinafuatwa bila kuvunjwa.
“Kampuni ya Sportpesa inatoa kiasi cha Mil.20 na jezi kwa timu ya Polisi Tanzania ambazo zitatumika katika shughuli mbalimbali ili kuimarisha timu hiyo kwani tumedhamiria kuendeleza na kukuza mpira wa miguu nchini kwa kutoa msaada kwa timu mbalimbali,” alisema Tarimba.
Aidha SportPesa wamekabidhi pia tuzo ya Certificate of Appreciation ikiwa ni ishara ya kuthamini mchango wa Jeshi hilo katika kusimamia ulinzi na usalama hasa wakati wa zaiara ya Klabu ya Everton hapa nchini ambayo ilikuja kucheza na Timu ya Gor Mahia ya Kenya.
Post a Comment