Simba Yakubali Milioni 10 za Buswita
Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi za wachezaji imesema haioni haja ya kuendelea kumfungia kiungo aliyesaini kandarasi katika vilabu viwili tofauti ambaye ni Pius Buswita baada ya yeye kukubali kuilipa Simba Milioni 10.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Elias Mwanjala leo baada ya vilabu hivyo kukaa pamoja na kufikiana muafaka juu ya mchezo huyo.
"Vilabu vya Simba na Yanga vimeshakaa na kuongea ambapo wamekubaliana mchezaji huyo arudishie pesa aliyoichukua ili aweze kufunguliwa lakini tumpe onyo kali ili suala hili lisiweze kujitokeza kwa mara nyingine", amesema Mwanjala.
Hata hivyo, Kamati ya hiyo imesema lengo hasa la kuridhia kumtoa kifungoni Pius ni kutokana na kuona mpira ndiyo ajira yake ambayo anaitegemea.
Kwa upande mwingine, Klabu ya Simba wamedai walipwe pesa ya nauli ya ndege waliyomlipia mchezaji huyo pindi wamemchukua ambapo Yanga wamekubali kuilipa pesa hiyo.

Post a Comment