KAHABA MZUNGU ATIKISA DAR! AHOFIWA KUSAMBAZA VIRUSI
DAR ES SALAAM: Kabaaang! Changudoa mmoja wa Kizungu raia wa Uholanzi aliyefahamika kwa jina moja la Monica ametikisa Jiji la Dar kwa kuwa gumzo na wateja wengi kumgombea, Risasi Mchanganyiko lina ‘full’ stori.
SNICHI AVUJISHA ISHU
Baada ya kutonywa, Kitengo Maalum cha Operesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers kilimnasa ‘live’ Mzungu huyo mchana kweupe akiwa kwenye moja ya ‘kiunga’ cha biashara hiyo haramu maeneo ya Kinondoni jijini Dar. “Hapo ni kitengo cha OFM? Mimi ni msomaji wa magazeti yenu, nina habari kutoka hapa mtaani kwetu kuna changudoa mmoja wa Kizungu kila siku huwa anajiuza mchana kweupe.
ANABONGA KISWAHILI
“Ukimuona ni Mzungu kabisa tena anaongea na Kiswahili safi utafikiri amezaliwa Tanzania, yaani nakwambia watu wanamchukua kwa bei chee, hebu njooni mumfungie kazi,” kilisema chanzo.
AHOFIWA KUSAMBAZA VIRUSI
Chanzo kiliendelea kutiririka kwamba, wakazi wa eneo hilo wana hofu isije ikawa Mzungu huyo akawa na virusi vya ugonjwa wa Ukimwi, hivyo kutojali kwa kuwabadilisha wanaume wengi kwa siku moja. “Hofu imejaa mtaani, kila mmoja haamini kama Mzungu wa kike tena mrembo kama huyu anaweza
kujiuza mchana kweupe kwa bei chee. Isije akawa ameathirika akawa anawasambazia vijana wetu, maana naona wanamchangamkia kweli,” kilisema chanzo hicho.
kujiuza mchana kweupe kwa bei chee. Isije akawa ameathirika akawa anawasambazia vijana wetu, maana naona wanamchangamkia kweli,” kilisema chanzo hicho.
WAUME ZA WATU WAMGOMBEA
“Bahati mbaya zaidi hata waume zetu siku hizi hawashikiki. Wanamgombea kwelikweli. Tunapata shida, wanamkimbilia mno, kwa staili hii unafikiri tutapona kweli?” MAKONDA UPO?
Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda ambaye amekuwa akipambana na biashara hiyo kama anadhani ameikomesha, aelewe tu bado tatizo lipo. “Makonda amekuwa akipambana sana na hawa wadada wanaojiuza, sasa sijui kama anajua sasa hivi Mzungu na Wabongo wengi tu wanajiuza mchana kweupe.
“Tunamuomba aingilie kati suala hili kwani nakumbuka baada ya kuelezea mafanikio aliyoyapata, changamoto alizokutana nazo na mipango inayofuata ya mwaka wake wa pili alisema atahakikisha anapambana na machangudoa wote katika mkoa huu,” kiliweka nukta chanzo hicho.
OFM ENEO LA TUKIO
Baada ya kupokea taarifa hiyo, OFM walifunga safari kwa siku mbili mfululizo katika kiunga hicho maarufu kwa Mzungu huyo kufanya biashara yake.
SIKU YA KWANZA OFM
Ilipofika siku ya kwanza, iliagiza vinywaji katika baa hiyo kisha kumsikilizia Mzungu huyo huku ikiomba maelezo kutoka kwa mmoja wa wahudumu wa baa hiyo. OFM: Ebhana kuna Mzungu huwa anajiuza hapa, vipi leo hajaja? Mhudumu: Bado ila ndiyo mida yake hii, vipi unamtaka nini? OFM: Yeah nina shida na huduma hiyo si unajua sijawahi ‘onja’ Mzungu. Mhudumu: Msubiri hapahapa, haiwezi kupita siku hajaja.
GHAFLA AIBUKA
Baada ya muda mfupi, Mzungu huyo aliingia na kwenda kuzungumza na baadhi ya wahudumu wa baa hiyo kisha kumlengesha kwa mteja mwingine, hivyo OFM kuambulia patupu.
OFM YAAMBULIA PICHA
Hata hivyo, OFM ilifanikiwa kumtandika picha Mzungu huyo akiwa amekaa kwenye meza na mteja mwingine kabla ya kuondoka naye na kutokomea kusikojulikana.
SIKU YA PILI SASA…
Siku ya pili yake kikosi kilitinga tena mchana na kuweka kambi na muda wa saa sita za mchana Mzungu huyo alitokea na kuitwa akiwa amechangamka mkononi ameshika kinywaji.
USO KWA USO NA OFM
Kwa kutokujua kama aliyekuwa akimuita ni OFM, ali
sogeza kiti na kuulizwa moja kwa moja kama anajishughulisha na biashara hizo ambapo alikubali. ATAJA BEI YAKE Huku OFM ikimrekodi mwanzo mwisho, ilianza ‘kubageni’ naye ambapo Mzungu huyo alichomoa simu yake ya mkononi kisha akaandika kiasi cha shilingi 80,000 na kumpatia OFM ashuke nayo mwenyewe. AKOMAA NA SH. 50,000 Baada ya kushushana bei na OFM kwa muda mrefu, Mzungu huyo alikubali yaishe kwa kuandika kiasi cha mwisho cha shilingi 50,000 na kusema kuwa ni kiwango cha mwisho kwake kuwatoza wateja wanaotaka huduma ya mwili wake.
sogeza kiti na kuulizwa moja kwa moja kama anajishughulisha na biashara hizo ambapo alikubali. ATAJA BEI YAKE Huku OFM ikimrekodi mwanzo mwisho, ilianza ‘kubageni’ naye ambapo Mzungu huyo alichomoa simu yake ya mkononi kisha akaandika kiasi cha shilingi 80,000 na kumpatia OFM ashuke nayo mwenyewe. AKOMAA NA SH. 50,000 Baada ya kushushana bei na OFM kwa muda mrefu, Mzungu huyo alikubali yaishe kwa kuandika kiasi cha mwisho cha shilingi 50,000 na kusema kuwa ni kiwango cha mwisho kwake kuwatoza wateja wanaotaka huduma ya mwili wake.
“Ndiyo nafika sasa, nisubiri kwanza nile chakula nilichoagiza halafu tutakwenda,” alisema Mzungu huyo bila papara akiweka miguu mapajani mwa OFM huku akipuliza sigara. MARA PAAP, GESTI!
Ili kujiridhisha zaidi kuwa anaweza kwenda gesti na kukubali kila kitu, Mzungu huyo alimaliza kula na kukodiwa Bajaj ambayo ilimpeleka akiwa na OFM hadi gesti moja maeneo ya Mwananyamala. …WAFIKA Makachero walioizingira gesti hiyo, walichukua matukio hatua kwa hatua hadi walipoingia chumbani ambapo alionesha kukubali kutoa huduma kwa kuanza kuvua nguo moja baada ya nyingine na alipomaliza kuvua zote, OFM alitumia mbinu ya kumdanganya kuwa amepigiwa simu ya dharura na kuvaa nguo zake na kutoka naye nje.
NENO LA MHARIRI
ni vyema serikali ikachukua hatua kukomesha biashara hii, lakini pia waume za watu na vijana mbalimbali wakawa makini na biashara hii kwani ni rahisi kupata maambukizi ya magonjwa endapo Mzungu huyo atakuwa ameathirika. Aidha, serikali inapaswa kufanya kitu ikiwezekana kumrejesha Mzungu huyo nyumbani kwao, kwani kama atakuwa ni mwathirika, ni rahisi kuwaumiza wengi kwa sababu tu ya uzungu wake.
Post a Comment