Header Ads

SAMATTA KAIZUNGUMZIA UGANDA YA KINA OKWI, MANENO YAKE HAYA HAPA...



Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, amesema kuwa, timu ya taifa ya Uganda, imejidhatiti vilivyo na tukikutana nayo hivi sasa lazima itufunge kutokana na ubora waliokuwa nao.

Samatta ambaye anaichezea Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, ameyasema baada ya hivi karibuni Uganda kuinyuka Misri bao 1-0 katika mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia, mwakani.

“Uganda wenzetu wapo vizuri kuliko sisi kwani ukiangalia hivi sasa wanapambana kuhakikisha wanashiriki Kombe la Dunia na wanafanya vizuri kwenye mechi zao.

“Ubora waliokuwa nao tukikutana nao wanaweza kutufunga kwani wapo juu sana dhidi yetu na ubora wao unawafanya kuwa kinara Afrika Mashariki na hakuna wanaowafikia,” alisema Samatta.

No comments