Header Ads

OKWI, OMOG SASA SAFI, WAENDELEA NA MAZOEZI SIMBA IKIJIFUA DAR

WACHEZAJI WA SIMBA WAKIMUANGALIA OKWI BAADA YA KUGONGANA NA OMOG

Kocha Joseph Omog na mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi, leo wameendelea na maazoezi kama kawaida.

Kuendelea kwa mazoezi kwa waili hao maana yake hali yao ni safi baada ya ile “ajali” ya jana mazoezini.

Okwi na Omog waligongana katika mazoezi ya jana kwenye Uwanja wa Uhuru wakati wa mazoezi ya timu hiyo.

Okwi alionekana yuko vizuri lakini Omog alilazimika kupata matibabu kidogo kutoka kwa dakari wa Simba.


Meneja wa Simba, Cosmas Kapinga amethibitisha wawili hao kuwa katika hali nzuri na kusema kila kitu kipo safi.

No comments