Header Ads

October 9 Vanessa Mdee ‘ulingoni’ kuwania tuzo 5 za kimataifa


Msanii wa muziki Bongo, Vanessa Mdee yupo mbioni kuanza safari ya kuwania tuzo tano tofauti za kimataifa.
Vanessa anawania tuzo zifuatazo;  AFRIMMA katika kipengele cha best Female East Africa, AFRIMA katika kipengele cha Best Female Artiste in Eastern Africa, EA Awards katika kipengele cha Best Female Africa Artist
Pia  anawania tuzo za Nigerian Entertainment Awards (NEA) katika kipengele cha Best Africa Female Artist [Non-Nigerian] na Africa Entertainment Awards (AEA) za Marekani katika kipengele cha Best International African Female Artist na Best International Artist.
“So zote zinatakiwa kura na tunaendelea kupambana kupiga kura, tuzo ya kwanza kabisa kutolewa ni October 9 (mwaka huu) ambayo ni ARIMA ya Marekani, so let try busy tuzirudishe nyumbani,” amesema Vanessa Mdee.
Ieleweke kuwa tuzo hizo zitatolewa kwa wakati tofauti ila ya kwanza ndio October 9, 2017. Vanessa Mdee kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Kisela’  ambayo amemshirikisha Mr. P (P square) kutoka nchini Nigeria.

No comments