Header Ads

KUN AGUERO AVUNJIKA MBAVU AJALINI


MSAMBULIAJI wa Klabu ya Soka ya Manchester City na timu ya taifa ya Argentina, Sergio Kun Aguero,amepata ajali ya gari usiku wa jana akiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege nchini Uholanzi ambako alikuwa amehudhuria tamasha la muziki. 
Kwa mujibu wa ripoti, Aguero, 29,amevunjika mbavu na atakuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili na atakosa mchezo dhidi ya mabingwawatetezi wa ligi kuu nchini Englandklabu ya soka ya Chelsea utakaopigwa Jumamosi hii.
Picha zilizosambaa katika baadhi ya mitandao kutoka nchini Uholanzizimeonyesha gari ndogo ambayo Agueroalikuwepo na dereva wake ikiwa imegonga nguzo katikati ya jiji la Amstedam huku ikiripotiwa kuwa hakuna aliyepoteza maisha zaidi ya kuumia.
Awali aliweka picha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii waInstagram ikimuonyesha yeye na msanii kutoka Uholanzianayefahamika kwa jina la Malumaambaye ndiye aliyemualika staa huyo wa Argentina katika tamasha hilo
Mpaka sasa Aguero ana mabao sita katika ligi kuu ya England.

No comments