Header Ads

Mapenzi ya kuachana na kusumbuana yapo kila siku – Lava Lava


Msanii wa Bongo Flava, Lala Lava amesema watu kutengana katika mahusiano ni jambo la kawaida ambalo hutokea kila mara na ndio sababu ya wimbo wake ‘Bora Tuachane’ kuendelea kufanya vizuri.

Muimbaji huyo kutoka WCB ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma- ameiambia Dj Show ya Radio One kuwa kitu hicho kitafanya ngoma hiyo kuwepo kwa wakati wote.
“Bora Tuachane ukizungumzia stori na ile melody na mashairi ni vitu ambavyo vinaishi miaka yote nafikiri, ndio maana nahisi mpaka leo ni wimbo unafanya vizuri na watu wanatumiana kwa sababu mapenzi ya kuachana na kusumbuana yapo kila siku, hayawezi yakaisha, kwa hiyo unaishi kutokana na ujumbe wake,” amesema Lava Lava.
Bora Tuachane ilikuwa ni wimbo wa kwanza kwa Lava Lava chini ya WCB kisha kufuatiwa na kolabo waliyofanya wasanii wote wa label hiyo.

No comments