Header Ads

Kama soka ni rekodi baasi leo United anashinda huku Chelsea anasuluhu


Katika michezo 8 iliyopita, Manchester United hawajawahi kupoteza na hii leo watajaribu kuendeleza rekodi hii mbele ya CSKA Moscow, mchezo ambao utaamua nani anaweza kuongoza group A.
Mchezo huu kama ni rekodi tu baasi United wana asilimia kubwa kushinda katika mchezo huu kwani michezo minne iliyopita dhidi ya CSKA Moscow hawajawahi kupoteza hata mchezo mmoja.
Na ukiacha tu United kutofungwa na CSKA Moscow lakini pia kocha Jose Mourinho tangu akiwa Real Madrid hajawahi kupoteza dhidi ya Moscow huku akiwa amewafunga mara 6 na kupata suluhu moja.
Kama ilivyo kwa Manchester United lakni vile vile Athletico Madrid nao leo wanavaana na Chelsea huku Wahispania hao wakiwa hawajawahi kufungwa na Chelsea katika michezo yao minne iliyopita.
Chelsea watakutana na upinzani mkali mno kwani Athletico ni wabishi sana nyumbani kwao, katika michezo 23 waliyocheza Hispania klabu hiyo imepata ushindi mara 18 rekodi inayoonesha utemi wao wakiwa nyumbani.
Pamoja na hayo lakini haitakuwa rahisi sana kwa Diego Simeone kwani The Blues hawajawahi kufungwa na timu za kutoka Hispania katika michezo 9 iliyopita ya ugenini katika Champions League wakishinda mara 2 na kusuluhu mara 7.
Ukiangalia rekodi za timu hizi mbili Athletico na Chelsea utagundua wanakutana katika mchezo huu huku hakuna mnyonge kati yao na viwango vyao vya sasa vinaonekana kuendana, jambo ambalo linaufanya mchezo huu kuwa wa pande zote.
Michezo mingine hii leo kutakuwa na mchezo kati ya Fc Basel watakaokuwa nyumbani kuikaribisha Benfica huku kundi C kutakuwa na mchezo kati ya As Roma watakaoifuata Quarabag Fk.

No comments