Header Ads

Majeruhi wa Simba watakaoikosa mechi Azam Jumamosi


Klabu ya Simba imewatoa hofu mashabiki wake kwa kutaja wachezaji wenye majeruhi kuelekea mchezo wao dhidi ya Azam. Hadi sasa klabu ya Simba ina wachezaji wawili wenye majeruhi ambao hawapo kwenye hesabu za kocha Joseph Omog.
Mratibu wa timu Abbas Ally amesema, Said Mohamed na Shomari Kapombe ni wachezaji pekee ambao hawapo kwenye mipango ya kocha kuelekea mchezo wao wa mwisho wa juma dhidi ya Azam FC.
“Majeruhi tulionao ni walewale tu ambao kimsingi hawapo katika program yetu, Said Mohamed ‘Nduda’ anaenda nje kwa ajili ya matibabu lakini Shomari Kapombe  ambaye alipata majeraha katika timu ya taifa bado hajaanza kufanya mazoezi. tunatarajia Jumatatu ataanza mazoezi chini ya uangalizi wa daktari”-Abbas Ally.
“Kikosi kipo kambini na kila kitu kinaendelea vizuri kama tulivyopanga tunaendelea na mazoezi, tutafanya mazoezi leo na tutamalizia mazoezi yetu ya mwisho kesho kabla ya mchezo wa Azam.”
Simba itacheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Jumamosi September 9, 2017 kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi saa 1:00 usiku.

No comments