Romelu Lukaku ameendelea kucheka na nyavu baada ya usiku wa leo kufunga bao la ushindi wakati Ubelgiji wakiifunga Ugiriki 2 kwa 1, bao lingine la Ubelgiji lilifungwa na Vertoghen huku bao la Ugiriki likiwekwa kimiani na Zeca.
Ureno waliibuka kidedea kwa ushindi wabao moja lilofungwa na Andre Silva dhidi ya Hungary huku Ufaransa wakitoka suluhu ya bila kufungana dhidi ya Luxembourg.
Iholanzi wakiwa nyumbani waliichabanga Bulgaria kwa mabao 3 kwa 1, mabao yakiwekwa kimiani na Arjern Robben pamoja na Davvg Proper aliyefunga mara mbili huku lile la Bulgaria likifungwa na George Kostadinov.
Kwa matokeo ya leo Ubelgiji wanafudhu kwenda fainali za kombe la dunia kwa mara ya 13, rekodi ambayo ni timu 5 tu za Ulaya zimewahi kufudhu zaidi ya idadi hiyo.