Header Ads

Hivi Kwanini Baadhi ya Watanzania Wanataka Diamond Aanguke Kimuziki?


Diamond Platnumz ni mwanadamu ana madhaifu yake kama alivyo binadamu yeyote yule. Lakini katika picha kubwa na kimuziki huyu ndugu yetu anaiwakilisha nchi vyema sana huko nje.

Nadhani hili ndilo la Msingi na tungebaki kuliangalia wote kama Watanzania. Kuwa na timu siyo makosa hata Yanga na Simba ni Wapinzani wakubwa lakini tukija kwenye Taifa Stars hizo timu tunazivua na tunavaa Utaifa. (Huu ndiyo Uzalendo jamani)

Utaifa ukiisha tunarudi kwenye timu zetu na kuanza kung'oa viti pale uwanja wa taifa. Hivyo basi kwenye kujenga sifa za wasanii wetu awe Ali Kiba, Diamond au Vanessa Mdee tushindane humu ndani lakini tusifanye chuki kiasi cha kutaka kuchafua sia zao. Hao ni watoto wetu kabisa,watoto wa nchi hii: Hakuna mzazi anayetup watoto jamani.

Tumtie moyo Alikiba na tumtie Moyo Diamond: Pia tuwakosoe pale wanapofanya vibaya hali tukiwa na dhamira safi kabiaa ya kutaka kuwajenga kimuziki. Tuepukane na fitna,majungu na uzandiki l: haya mambo hayajengi kabisa. 

No comments