Header Ads

Dortmund waweka rekodi Bundesliga huku Pep Gurdiola “akivunja” daraja Epl


Haikuwa siku nzuri kwa Antonio Conte na mbinu za Pep Gurdiola zilimpoteza kabisa, ilikuwa mbaya kwa Chelsea kwani ndio mchezo wa kwanza kwa Chelsea kupiga mashuti machache.
Chelsea hawajawahi kupiga mashuti yaliyolenga bao chini ya 5 tangu Conte ajiunge nao, lakini hii leo wamepiga mashuti manne tu huku kuanzia dakika ya 26 hadi mpira unaisha walipiga mashuti mawili tu.
Manchester Citu walipata bao lao la kwanza na la pekee kupitia kwa Kelvin De Bruyne na kuwafanya sasa kuwa wamecheza michezo minne mfululizo wakishinda bila kuruhusu bao katika Epl.
Kule nchini Ufaransa Kylian Mbappe alifunga moja ya bao katika ushindi wa bao 6 kwa 2 dhidi ya Bordeaux na kumfanya kinda huyo kuhusika katika mabao 29 ya ligi ya Ligue 1 msimu huu akifunga 14 na kuasisst 5.
Ushindi huo wa PSG umewafanya kufikisha idadi ya michezo 28 nyumbani bila kupoteza mchezo hata mmoja huku wakisuluhu 6 na kushinda mechi 22, mabao mwngine yalifungwa na Neymar (2), Cavanni na Thomas Meunier.
Bundesliga nako Borussia Dortmund walishinda bao 2 kwa 1 dhidi ya Augsburg ikiwa ni mchezo wao wa 6 msimu huu na kumfanya kocha Peter Bosz kuwa kocha wa kwanza katika ligi hiyo kushinda michezo 6 kati ya 7 ya mwanzo katika Bundesliga.

No comments