Arsenal na Chelsea wafanya kitu kilichowashinda Manchester United katika usajili
Usajili nchini Uingereza umefungwa rasmi usiku wa Alhamisi, timu nyingi zilifanya manunuzi makubwa hali iliyopelekea vilabu 14 vya ligi hii kuvunja rekodi yaonya usajili ambayo iliwekwa na wachezaji wengine hapo mwanzo.
Arsenal, wakati Mesut Ozil ananunuliwa kwenda Gunners mwaka 2013 ndio aliweka rekodi ya usajili ghali baada ya kununuliwa kwa £42m toka Real Madrid lakini ujio wa Alexandre Lacazzete toka Lyon kwa £53m umevunja rekodi ya Ozil.
Tottenham Hotspur, Davinson Sanchez amenunuliwa kwa £42m kutoka Ajax na hii imevunja rekodi ya Moussa Sissoko na Eric Lamela ambao walinunuliwa kwa £30m katika misimu iliyopita.
Chelsea, Fernando Torres alienda Chelsea kwa ada ya £50m lakini rekodi yake imekuja kuvunjwa na Mhispania mwenzake Alvaro Morata ambaye Chelsea walimnunua kwa £70m kutoka Real Madrid.
Liverpool, usajili wa Mohamed Salah kutoka As Roma kuja Liverpool ulionekana wa pesa nyingi baada ya Liva kutumia £36m kumnunua, lakini Nady Keita amevunja rekodi ya Salah baada ya ununuzi wake kutoka Red Bull Leizpg kuigharimu Liverpool kiasi cha £55m.
Everton, msimu huu wamefanya sana manunuzi lakini uhamisho wa Gylfi Sigurdsson kutoka Swansea umeifanya klabu hiyo kuvunja rekodi ya Jordan Pickford aliyenunuliwa kwa £30m, Sigurdsson amenunuliwa kwa £45m.
Lakini kuna vilabu bado rekodi zao kubwa za usajili zimeshindwa kuvunjwa Manchester City wameshindwa kuvunja rekodi ya De Bruyne (£54m) huku Manchester United nao wakishindwa kuvunja rekodi ya Paul Pogba (£89m).
Post a Comment