Header Ads

UKARIBU NA BELLA UMENIBEBA!


MSANII wa Bongo Fleva, Pamela Daffa ‘Pam D’ amefunguka kuwa, ukaribu alionao na staa wa Muziki wa Dansi, Christian Bella ‘Obama’ umembeba kwa kiasi kikubwa.
Akistorisha na Over Ze Weekend, Pam D anayebamba na Wimbo wa Ngoma Droo akiwa amemshirikisha Bella, alisema tangu kutoka kwa wimbo huo amekuwa akizunguka na Bella sehemu nyingi kwa ajili ya kuutambulisha japokuwa amekuwa akikutana na changamoto za hapa na pale za kuhisiwa huenda wameanzisha uhusiano.
“Liko wazi, Bella amenibeba sana, nashukuru kwa hilo. Wapo wanaohisi tofauti baada ya kutoa wimbo huu kwa sababu nakuwa naye karibu kote anapokwenda,” alisema Pam D.
OVER ZE WEEKEND

No comments