Header Ads

Romelu Lukaku aiweka Manchester United kileleni huku Samatta naye akifunga mara mbili Genk


Manchester United wamekaa kileleni mwa ligi huku furaha kubwa kwa mashabiki wa klabu hiyo ni kuona nyota wao wawili wapya Romelu Lukaku na Nemanja Matic wakifanya vizuri katika mchezo wa leo dhidi ya West Ham.
Alikuwa Romelu Lukaku dakika ya 33 alifunga la kwanza na 52 akafunga lingine kabla ya Anthony Martial aliyetokea benchi kufunga la tatu na Romelu Lukaku katika dakika ya 90 akafunga bao la nne.
Kiungo Nemanja Matic aliibuka mchezaji bora wa mechi huku Romelu Lukaku mabao yake yanamfanya kuifunga West Ham jumla ya mabao 11 na timu hiyo inakuwa timu aliyoifunga zaidi.
Kabla ya mchezo huo Tottenham Hotspur walikuwa uwanjani dhidi ya Newcastle United huku Tot wakiibuka kidedea kwa mabao mawili kwa sifuri kwa mabao yaliyofungwa na Delle Ali na Ben Davies.
Katika ligi ya Ubelgiji Mtanzani Mbwana Samata alifunga mara mbili na kuisaidia klabu yake ya Krc Genk kuibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 5 kwa 3 dhidi ya klabu ya Royal Antwerp.
Mabao mengine ya Genk yalifungwa na Leandro Trosward, Shrijives huku Dino Arslaganic akijifunga, mabao ya Antwerp yakifungwa na Dequevy, William Owosu na Dino Arslaganj
Kule Ligue One Monaco walikuwa uwanjani dhidi ya Dijon na mshambuliaji wao Radamel Falcao akifunga hatrick katika ushindi wa mabao manne kwa moja, bao lingine la Monaco lilifungwa na Jemerson huku lile la Dijon likifungwa na Wesley Said.

No comments