Header Ads

TID: SIJARUDIA MADAWA JAMANI


MKONGWE kunako Muziki wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed ‘TID’ amewajia juu wanaoendelea kumhusisha kurudia matumizi ya madawa ya kulevya kwa kusema kuwa hakuna kitu kama hicho na wanaoeneza taarifa hizo wana lengo la kumchafua tu.

Akipiga stori na Ijumaa, TID ambaye kipindi kifupi cha nyuma aliwahi kukiri kutumia madawa alisema, alishatangaza ameacha mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda hivyo hawezi kurudi nyuma akatumia tena hivyo vitu.

“Sijarudia jamani, hayo mambo ni ya uchochezi hakuna la zaidi, nimeshaacha hayo mambo kwa nini watu wanizushie, sijarudia madawa,  cha muhimu ni kujua mikakati ya kazi zangu kimuziki ndio ninachowaza si hayo mambo. “Sina cha kuwashauri wasanii wanaoendelea kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, sababu nilishaongea mengi tangu awali nilipotangaza nimeacha,” aliongeza TID.

No comments